July 2, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Simba kimeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya KAGAME baada ya kuwafunga APR ya Rwanda kwa mabao 2-1.

Katika mchezo huo uliokuwa na mashambulizi ya zamu kwa zamu, ulimalizika dakika 45 za kwanza bila timu yoyote kuona bao.

Mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilionesha kukamiana zikiwa na lengo la kucheka na nyavu ambapo mnamo dakika ya 66, Kinzingabo aliweza kuiandikia APR bao la kwanza.

Ilichukua takribani dakika 6 baadaye Simba kuweza kusawazisha ambapo katika dakika ya 72, mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa, Adam Salama alifunga na kuufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1.

Wakati mpira ukiwa katika dakika za nyongeza, straika hatari mpya, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la pili na la ushindi kwa njia ya penati baada ya kuangushwa katika eneo la hatari.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Simba walikuwa mbele kwa mabao 2 na APR kutoka Rwanda wakiwa na 1.

5 COMMENTS:

  1. Aliyeangushwa sio ndemla alikuwa kagere

    ReplyDelete
  2. Aliyetoa pasi ndio Said Ndemla aliyepokea pasi kutoka kwa Wawa.

    ReplyDelete
  3. Hii blog kuchapia si mara ya kwanza badilikeni jamani mmmh...! pia kabla hamjarusha taarifa mtandaoni jiridhisheni kwanza ni hayo tu kwa leo

    ReplyDelete
  4. Hata paragraph ya mwisho matokeo ameondoka Simba 2 APR 0 badala ya Simba 2 APR 1.Hamna editing bora liende .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic