July 3, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Mtibwa Sugar kimewaongezea mkataba wa miaka miwili wachezaji wake Dickson Job na Kibwana Shomari.

Wachezaji hao wote wanaichezea timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys ambapo Job ni Nahodha na Shomari anacheza nafasi ya ushambuliaji.


Mtibwa wameamua kuingia kandarasi ya miaka miwili na wachezaji hao kwa ajili ya sehemu ya maandalizi kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19.

Mbali na msimu mpya kuelekea Ligi Kuu, Mtibwa itakuwa ainakabiliwa na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni baada ya kutwaa ubingwa wa FA kwa kuifunga Singida United mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.

Wachezaji hao watakuwa na Manungu Complex mpaka mwaka 2020.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic