July 3, 2018


Wakati sekeseke la usajili hapa Tanzania likizidi kushika kasi kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, imeelezwa mabosi wa Simba tayari wameshamalizan na kiungo wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema kuwa Kamati ya Usajili imeshamaliza kufanya mazungumzo na Dilunga na kufikia makubaliano na kilichobaki ni kupewa mkataba wa kusaini.

Dilunga ameelezwa kumalizana na Simba ikiwa ni siku kadhaa zilizopita iliripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na timu yake ya zamani ya Yanga lakini inaonekana wameanza kupigwa kete na watani zao wa jadi Simba.

Simba wameanza harakati za kuanza kuimarisha zaidi eneo la kiungo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano ya kimataifa ya CAF ambapo itakuwa inaiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika kikao kilichoitishwa mara ya mwisho mbele ya waandishi wa habari, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, alifunguka na kusema Kamati ya Usajili itaendelea kufanya usajili kulingana na mapendekezo ya Kocha.

Hatua hii waliyofika nayo Simba kwa Dilunga, unakuwa unawapa wakati mgumu watani zao wa jadi Yanga ambao nao wanawania saini yake, kutokana na jeuri ya fedha za Mohamed Dewji kwa wekundu hao wa Msimbazi

3 COMMENTS:

  1. Dah tuoneeni huruma...tunaomba poa

    ReplyDelete
  2. Yanga fanyeni hivi chagua majina Fulani msio wahitaji,muwataje taje, kisha hao jamaa kwakuwa wanataka sifa wakawajaze pale mwisho wa siku wakauze nyanya.

    ReplyDelete
  3. Si mlikuwa munawaonea Simba. Kisasi ni haki, wamepanda na sasa wanakivuna, wala hakuna cha ajabu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic