July 4, 2018


Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera amejiridhisha kwamba straika Heritier Makambo na Mrisho Ngassa wana uwezo wa kucheza Yanga msimu ujao na amewaambia viongozi wawape chao.

Makambo ametokea DC Motema Pembe ya DR Congo na Mrisho Ngassa aliyekuwa Ndanda.

Siyo hao tu, pia Zahera amepitisha usajili wa kiungo rasta wa Majimaji, Jaffary Mohammed.

Usajili huo umepitishwa siku chache tangu wache­zaji hao wajiunge na Yanga kwenye mazoezi ya pamoja katika Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam ambako hakuna shabiki anayeruhusiwa kutia mguu kushuhudia.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Cham­pioni Jumatano, kocha huyo tayari amewapitisha wachezaji hao baada ya kuvutiwa na viwango vyao na akapukutisha wengine 25 waliokuwa na viwango vya kiujanja ujanja.

Mtoa taarifa huyo alisema, kikubwa kinacho­subiriwa kwa wachezaji hao ni kuandaliwa mikataba na kusaini na tayari fungu la usajili limetua kwenye akaunti ya klabu.

“Makambo, Ngassa na Jaffary anayecheza kiungo namba sita aliyekuwa Maji­maji, ndiyo waliopitishwa.

“Hivyo, kama mambo yakikaa sawa wakati wowote watasaini mi­kataba kwani majina yao tayari kocha ameyakabidhi kwenye kamati husika ya usajili,”alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza kwamba Kocha amewaambia viongozi wasiumize kichwa mambo yatakuwa biyee.

Alipotafutwa Zahera kuzungumzia hilo, alisema: “Tayari nimepitisha majina ya wachezaji watatu pekee, hivyo mara baada ya kuka­milika kila kitu katika usajili huo uongozi utatangaza rasmi majina yote.”


CHANZO: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Wazee wa Kimyakimya vipi mbona mnaanza kupiga kelele, hamumuogopi Mnyama!

    ReplyDelete
  2. Wakati mwingine magari ya mkaa ndo huwa yanaokoa wasafiri wakati wa mkwamo kutokana na njia kuwa mbovu na watu wakaendelea na safari

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic