July 1, 2018


HISPANIA wameshindwa kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuchapwa na Urusi kwa penalti 4-3 kwenye mechi iliyopigwa dakika 120 leo.

Mchezo huo ulikwenda kwenye penalti baada ya sare ya bao 1-1 kwa dakika zote 120. Hispania walimiliki mpira kwa asilimia 71 kipindi cha kwanza cha mchezo huo, lakini walienda mapumziko wakiwa sare ya bao 1-1.

Beki wa Urusi, Sergei Ignashevich anayeichezea CSKA Moscow, aliendeleza wimbi la timu yake kujifunga baada ya kujaribu kuokoa mpira uliopigwa na Marco Asensio, huku akipambana na Sergio Ramos lakini akaugonga ukaingia wavuni.

Baada ya bao hilo, Hispania waliendelea kutawala mchezo huo lakini walifanya kosa katika dakika ya 41, ambapo Gerrard Pique aliunawa mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi kuamuru penalti ambayo ilipigwa na Artem Dzyuba na kuipatia timu yake bao la kusawazisha.

Warusi wenyewe walifunga mikwaju yao kupitia kwa Fyodor Smolov, Pavel Ignatovich, Aleksandr Golovin na Denis Cheryshev na kutinga hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza kwenye rekodi yao. Urusi anatarajiwa kukutana na mshindi kati ya Croatia na Denmark waliocheza usiku wa leo
Spain (4-2-3-1): De Gea 6; Nacho 6.5 (Carvajal 70, 6), Pique 7, Ramos 7, Alba 6.5; Koke 5, Busquets 5; Silva 4.5 (Iniesta 67, 6.5), Isco 7, Asensio 6.5; Costa 6 (Aspas 80).
Subs not used: Arrizabalaga, Reina, Saul, Thiago, Lucas, Odriozola, Azpilicueta, Monreal
Manager: Fernando Hierro 5
Goals: Ignashevich OG (12)
Russia (5-3-1-1): Akinfeev 9; Mario Fernandes 7, Kutepov 7.5, Ignashevich 7, Kudriashov 7, Zhirkov 6 (Granat 46, 7); Samedov 6.5 (Cheryshev 6, 61), Zobnin 7, Kuziaev 6.5 (Erokhin 6, 97); Golovin 7; Dzyuba 7 (Smolov 65, 6)
Subs not used: Lunev, Gabulov, Semenov, Gazinsky, Dzagoev, AL Miranchuk, AN Miranchuk
Manager: Stanislav Cherchesov 9.5
Goals: Dzyuba (41)
Referee: Bjorn Kuipers 6.5

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic