July 1, 2018


RAIS John Magufuli leo amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kwa mujibu wa taarifa yake iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

Kangi Lugola, aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) sasa anakuwa  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo amechukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.

Nchemba ni mwanamichezo maarufu kwa kuwa ni shabiki wa Yanga, Singida United pia mshambuliaji wa timu ya Bunge.

Musa Ramadhani Sima amekuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

Omary Mgumba anakuwa  Naibu Waziri wa Kilimo.

Prof. Makame Mbarawa aliyekuwa Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anakuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

Mhandisi Isack Kamwelwe anakuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Athumani Kihami ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

7 COMMENTS:

  1. Unamaanisha nini kuandika anayeishabikia Yanga aondolewa;ni mawaziri wangapi ambao ni mashabiki wa Yanga au Simba waliondolewa kwenye baraza la mawaziri lakini hukuandika kama ulivyoandika habari hii.
    Yaani habari hata ikiwa inamuhusu mkeo utaweka jina la Yanga ili mradi tu.

    ReplyDelete
  2. Nimeamini huyu mwandishi ni mjinga wa mwisho. Anayeishabikia Yanga aondolewa. Ina maanisha kuwa ameondolewa kwa sababu yeye Yanga au? Tafuta cha kuandika jamaangu!!!

    ReplyDelete
  3. Dah angalau.... Nchemba kusema ukweli sikuwa na imani naye

    ReplyDelete
  4. Haya magazeti ya michezo yamevamiwa....hivi wamiliki wa hivi vyombo mbona mko kimya, kuondolewa waziri kuna uhusiano gani na sababu ya kuachwa Je ameondolewa kwakuwa ni Yanga au? Mbona kuna ambao ni Simba waliwahi kuachwa kwenye uwaziri na hamkuweka jina la Simba. Muwe waadilifu katika kazi zenu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Serikali ikiwadaabisha wanasema inaingilia na kuminya uhuru wa vyombo vya habari wakati umbulula wao ndo unapelekea kuadhibiwa na vyombo vya kusimamia maadili ya uandishi wa habari.

      Delete
  5. Hili jamaa ni kubwa JINGA hasa, yeye akili yake ni usimba tu. mpuuzi kabisa wewe mwandishi uchwara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic