July 1, 2018


Imeelezwa kuwa makipa wawili wa klabu ya Simba ambao wakuweza kutumika ipasavyo katika msimu wa ligi uliomalizika, Said Mohamed na Emmanuel Mseja wanaweza kutolewa kwa mkopo.

Taarifa za ndani kutoka kwa wekundu wa Msimbazi zinaeleza kuwa mabosi wa timu hiyo wamepanga kuwapeleka Mohamed na Mseja katika klabu nyingine ili kuwapana nafasi ya kujenga zaidi viwango vyao.

Nafasi kubwa kubwa ya kuondoka kwa makipa hao ipo kutokana na kukosa mechi za takribani mzima wa ligi uliomalizika.

Uongozi wa Simba ulifika hatua ya kumsajili kipa wake wa zamani, Deogratius Munish 'Dida' kwa ajili ya kumpiga tafu Aishi Manula ambaye atakuwa anafungua milango ya Mseja na Mohamed kuondoka kwa mkopo.

Simba hivi ipo katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (KAGAME) ambapo kikosi chake jana kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dakadaha FC kutoka Somalia.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic