July 1, 2018


Usajili umeendelea kushika kasi kwa klabu za soka Tanzania ambapo uongozi KMC umetangaza kumalizana na aliyekuwa beki wa Mbao FC, Sadala Mohamed.

Mohamed ametua Mbao kuungana na wakongwe kama Juma Kaseja kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

KMC ilifanikiwa kupanda daraja kushiriki Ligi Kuu msimu ujao imekuwa ikisajili wachezaji wazoefu ili kukiimarisha kikosi hicho kwa maandalizi ya ligi.

Mohamed aliyekuwa akiichezea Mbao amekuwa mchezaji wa pili kujiunga na KMC baada ya Yusuf Ndikumana kumalizana na klabu hiyo kwa pendekezo la Kocha Etienne Ndayiragije.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic