Wanachama wa klabu ya Simba katika tawi la Wekundu wa Mtogole lililopo Tandale wamelishukuru Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuatia kitendo cha kuwakumbushia Simba suala la uchaguzi mkuu.
Katibu wa tawi hilo anayejulikana kwa jina la Ponda, amesikika akizungumza kuwa TFF imefanya kitu kizuri kutokana na kuikumbushia katiba ya 2014 kuwa ndiyo inayotambulika tofauti na ya 2016.
Ikumbukwe juzi TFF walisema wao kama baba wa soka la Tanzania wanaitambua katiba ya Simba ya mwaka 2014 kuwa ndiyo inatambulika kwa chaguzi zote zilizopita na si ya 2016.
Ponda amesema TFF wamefanya jambo jema kwani hata siku za uchaguzi kuelekea uchaguzi zimeshafika huku akieleza kuwa uongozi wa Simba ulikuwa upo kimya.
Kiongozi huyo amefunguka na kuelezea hisia zake juu ya kamati ya uchaguzi TFF akiishukuru kutokana na kuwakumbushia Simba suala la katiba pamoja na uchaguzi kuwa umefika.
Klabu hiyo inatarajiwa kuanza harakati za uchaguzi ili kupata viongozi wengine watakaoingoza Simba kwa miaka minne ambapo kufikia mwishoni mwa mwezi wa saba utawala uliopo madarakani utakuwa umeshamaliza muda wake.
CHANZO: RADIO ONE
Blog yako natumika cvyoo.
ReplyDeleteKatika suala la uchaguzi ni vyema Mo Deuji ambaye kaiweka Simba katika hali hii ya juu ya kuheshimika kwa kujipanga kwa kila aina pamoja na kufungiwa milango wadokoaji na wapika majungu na kuifanya timu kuheshimika hata kumfanya mheshimiwa Raisi Magufuli kumvutia na kutowa maelekezo yake na kuamini timu itafanya kitu ambacho timu yeyote haijanta. Imekywa timu ta kutisha na kuheshimika kufikia Watani waliokuwa wakiionea Simba kujitowa Kagame kwa kumuogopa Mnyama. Sifa zimuoendee Mo na wasaidizi wake. Kqa kila aina ta ukweli na hisia za mashabiki, Mo awe awe Raisi wa kuliongoza jahazi kwani anasrahaki
ReplyDeleteHizi ni chokochoko za kutaka kuvuruga hatua za kuelekea kwenye maendeleo na kuachana na tegemezi na wapigaji.Wito wangu wanachama waliopitisha katiba ya 2016 basi wahakikishe wanaenda kupiga kura ya kuwabwaga hawa wachochezi.
ReplyDelete