July 4, 2018



Na Mwandishi Wetu
Watoto wa Kitanzania, Laigwanani Mollel na Ziporah Godfrey Mollel walioshiriki michuano ya soka kimataifa ya Football for Friendship (F4F) wameondoka Urusi kurejea Tanzania wakiwa na ndoto ya kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Dunia siku moja.

Michuano hiyo ya F4F ilishirikisha watoto wenye miaka 12 kutoka nchi 211 na imefanyika kwa mwaka wa sita tangu kuanzishwa kwake.

Laigwanani na Ziporah wakitokea akademi ya Lengo Football ya Arusha Tanzania wameondoka Urusi kurejea Tanzania wakisema ndoto yao kubwa ni kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Dunia siku za usoni.


“Niiwakilisha vizuri Tanzania kwa kupeperusha bendera ya taifa kwenye sherehe za ufunguzi wa Kombe la Dunia mwaka huu, ilikuwa kabla ya mechi ya ufunguzi ya Urusi na Saudi Arabia.

“Nilikuwa na uchovu sana baada ya kazi ya siku ile lakini naamini nimepata hamasa ya kuiwakilisha nchi yangu katika Kombe la Dunia siku zijazo kwa mimi mwenyewe kucheza uwanjani,” alisema Laigwanani.

Kwa upande wake, Ziporah alisema; “Nitakua na faraja sana kwa sababu Tanzania haijawahi kufuzu katika fainali za Kombe la Dunia, hivyo nitakuwa ni mimi ninaye iwakilisha nchi yangu.

“Nitajisikia ujasiri na nitaiwakilisha nchi yangu vizuri na najua katika mawazo yangu kuwa siku moja Tanzania itakuwa hapa katika fainali za Kombe la Dunia.”


Program hii ya Kijamii ya F4F ni programu ya kijamii inayojumuisha siku tatu za mafunzo ya soka na kila timu kati ya timu 32 kutoka duniani kote zilizipewa majina ya wanyama walio hatarini kupotea.

Timu zilizoundwa zilijumuisha wachezaji kutoka kila pembe ya dunia, kutoka mataifa makubwa na wadogo bila kujali, dini, tamaduni na ushawishi wa kisiasa na wa kiitikadi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic