July 4, 2018




Mabosi wa Kagera Sugar wamefanikiwa kuwaongeza mkataba,  kocha wake Mecky Maxime pamoja na beki wa timu hiyo, Juma Nyosso kwa muda wa mwaka mmoja iliweza kuimarisha kikosi hicho kwa msimu ujao.

Kagera ilimaliza katika nafasi ya tisa ikiwa chini ya kocha Maxime, ambapo awali ilionekana kusuasua na baadaye iliweza kurudi kwenye mstari na kupambana.

Katibu wa timu hiyo, Salum Madaki, alisema kuwa wameamua kuwapa mikataba hiyo kutokana na utendaji wao mzuri wa kazi ambao walionyesha msimu uliopita.

“Kocha tulimuongezea mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kufanya kazi na sisi  na kwa sasa amewasilisha ripoti kwa uongozi kwa ajili ya wachezaji ambao awahitaji na wachezaji ambao walikuwepo awali ambao ameamua kubaki nao tumewaongeza mkataba kama Nyosso kuna wengine tuliwahitaji ila tayari wameondoka kama Mohamed Fakh na Juma Kaseja,” alisema Madaki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic