WAZEE WA SAMBA KUKIPIGA NA MEXICO KOMBE LA DUNIA LEO
Vita ya kombe la Dunia inaendelea tena leo katika hatua ya 16 bora huku Urusi ambapo Brazil itakuwa inacheza dhidi ya Mexico majira ya saa 11 jioni.
Timu hizi zimekuwa zimekuwa zikileta msisimko wa aina yake kila pale zinapokutana ambapo mechi huwa ya aina yake na mara nyingi huwa na ugumu wa kipekee.
Rekodi zinaonesha Brazil imekuwa ikiibuka mbabe katika mechi nyingi ilizocheza dhidi ya Mexico, na leo wanakutana kufuzu kutoka 16 kuelekea robo fainali.
Brazil inashuka dimbani ikiwa na nyota wake wakali akiwemo Philippe Coutinho huku Mexico ikijivunia kuwa na Javier Hernandez 'Chicharito'.
0 COMMENTS:
Post a Comment