KIMYAKIMYA YANGA YASHUSHA STRAIKA HATARI KUTOKA NIGERIA, ANAKIPIGA SERBIA
Klabu ya Yanga imemsusha mshambuliaji Emeka Emarun kutoka Nigeria kwa kuja kumalizana na mabosi wa timu huyo kusaini mkataba, imeelezwa.
Emarun ambaye anaichezea klabu ya FK Radnick Pirot ya Serbia, inaelezwa amewasili usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kumalizana na viongozi wa Yanga.
Straika huyo anapewa nafasi ya kuchukua majukumu ya Donald Ngoma baada ya kuondoka na kuelekea Azam ambapo pengo lake ndani ya Yanga halijazibika mpaka sasa.
Mapema baada ya kuwasili Dar, mabosi wa Yanga wameamua kumficha mchezaji huyo ili kufanya naye mazungumzo ya siri ili kuweka kila kitu sawa kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba.
Ujio wa mchezaji huyo Dar ni kutokana na Kamati Maalum ya Mpito iliyo chini ya Abbas Tarimba ambayo awali ilisema itakuwa inafanya usajili wake kimyakimya.
Simba kitu hicho lakini wenyewe wanaita kimyakimya. Muwaheni huyo kabla kuingia mtego wa Yanga wakashindwa kumpa chake cha kila mwezi
ReplyDeletesaaa kikyakikya gani wakati ushasema hakuna siri tanzania bwana tutaona mwishowake
ReplyDeletesimba watachukua wachezaji wangapi wakati wachezaji wa nje walioruhusiwa ni saba tu !!! sidhani kama kila mchezaji anaetaka kusajiliwa na yanga ni mzuri !! kama ni kweli basi hongera yao yanga!!
ReplyDeleteUSANII TU, WATU WAMESHAZOEA CHANGA LA MACHO,....HAKUNA KINACHOENDELEA....NYIE SUBIRINI TU WATU WAANZE KUCHAPA BAKORA HAPO YANGA HAKUNA CHA KOCHA WALA NANI....WATU HAWATAVUMILIA UZEMBE MWAKA HUU
ReplyDeleteYANGA WASIPOANGALIA WANAWEZA WAKAFANYA VIBAYA KWENYE MCHEZO WAO NA GOR MAHIA ZIMEBAKI WIKI MOJA NA NUSU LAKINI BADO ASILIMIA KAMA 70% YA WACHEZAJI WA KIKOSI CHA KWANZA HAWAJAANZA MAZOEZI, WENGI WAO WAKIWA WANADAI MISHAHARA NA MIKATABA MIPYA AMBAYO BADO HAWAJAPEWA HII NI HATARI SANA, MWALIMU AMEANZA MAZOEZI NA KUNDI KUBWA LA WACHEZAJI WAPYA WANAOJARIBIWA, HII NI HATARI SANA, HATA HUYO MANJI KAMA ANA NIA NZURI YA KUISAIDIA YANGA KWANINI ASIRUDI TU KWENYE KAZI NA KUWALIPA MADAI YA WACHEZAJI? HIVI YEYE ATAFURAHI IKIWA TIMU HAITASAFIRI KWENDA KENYA KWAKUWA WACHEZAJI WAMEGOMA?? KWELI KAMA NIA YAKE NI NZURI KWANINI AISIINGILIE KATIKA WAKATI HUU AMBAPO MUDA UNAZIDI KWISHA, NA HAO WACHEZAJI HATA MAZOEZINI HAWAENDI??? HIVI HIYO KAMATI KWANINI HAIFANYI YALE WALIYOAMBIWA WAYAFANYE KATIKA MKUTANO MKUU? MUDA UNAISHA NA HAKUNA LINALOENDELEA NI VURUGU TUPU? HIVI KOCHA KWANINI ANAWAKATAA WACHEZAJI WANAOJARIBIWA? NA KWANINI HATA WANACHAMA HAWAUSHINIKIZI UONGOZI WAFANYE JUU CHINI WACHEZAJI WAANZE MAZOEZI HARAKA KWANI MUDA UNAISHA????
ReplyDelete