50 CENT, TEKASHI69 WARUSHIWA RISASI WAKISHUTI VIDEO
Marapa Tekashi69 na 50 Cent, wote wa Marekani, walipata taharuki juzi (Jumanne) wakati wakishuti video ya muziki eneo la Brooklyn, New York, ambapo mtu mmoja aliyekuwa katika gari aina ya Porsche jeupe, alirusha risasi 11 usiku mnamo saa 4:30.
Hata hivyo, risasi hizo zilizokuwa zikitoka kwenye gari hilo, hazikumdhuru mtu yeyote.
Marapa hao walikuwa pia na wanamuziki Casanova na Uncle Murda katika kushuti video hiyo.
Polisi hawajamkamata yeyote aliyehusika na kitendo hicho, japokuwa kuna wakati mwanamuziki Chief Keef, aliwahi kurushiwa risasi baada ya kutokea bifu kati yake na Tekashi.
0 COMMENTS:
Post a Comment