August 16, 2018


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekanusha taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini kwamba katika uchaguzi mdogo uliofanyika Agosti 12, mwaka huu uligubikwa na vurugu na uvunjifu wa sheria.



Aidha, tume pia imeutaka ubalozi huo kuthibitisha wanachokieleza juu ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu na kata 36.

Kwa mujibu wa taarifa ya NEC iliyotolewa na Ofisa Habari Mwandamizi wa tume hiyo, Christina Njovu, Ubalozi huo umetoa taarifa inayotoa tuhuma dhidi ya serikali, tume na jeshi la polisi kuwa sheria haikufuatwa na pia ulikuwa na vurugu katika uchaguzi huo.

“Uchaguzi mdogo huwa hauna waangalizi wa kimataifa, je ubalozi huo umetoa wapi taarifa hizo? Na hayo waliyoyaona, wameyaona kwa kutumia utaratibu upi na sheria ipi?

“Katika Jimbo la Buyungu mgombea wa ubunge mmojawapo kupitia Chadema alijitokeza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na kueleza hisia zake na kusema bayana kuwa amekubaliana na matokeo na ameshukuru kwa kuwa uchaguzi huo umemjenga.

“Kilichotokea Arusha ni vurugu mitaani mbali na maeneo ya vituo vya kupigia kura, kwa kuwa vurugu hizo zilipelekea jinai kufanyika vyombo husika vinashughulikia.

“Aidha, tume inapenda kuufahamisha umma kuwa Tanzania ni nchi huru na inaendesha chaguzi zake kwa mujibu wa katiba yake na sheria za uchaguzi. Kama kuna ambaye hajaridhika bado sheria za nchi zinampa fursa ya kuwasilisha malalamiko yake kwenye mamlaka mbalimbali zilizopo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.



3 COMMENTS:

  1. Hee hiyo nayo ni habari ya michezo?

    ReplyDelete
  2. Iwe habari ya michezo au isiwe linapokuja suala la uzalendo kwa nchi yetu tuplia mbali lazima tuoneshe kuumizwa pale tunapoona uhuru wetu kama taifa huru la kujiamulia mambo yetu yapo hatarini na mpongeza sana muandishi kwa kufikisha ujumbe kwani hii ni miongoni mwa Blog kubwa inayosomwa na watu wengi sio wanamichezo peke yao. Kwakweli utaona labda kwa baadhi ya watanzania vibaraka wanaojikweza kwa vibaraka kuleta fitna ndani ya nchi na kuipaka matope nchi yetu kimataifa na duniani au Ubabe wa mataifa makubwa kutojali uhuru wa mataifa machanga wa kujiamulia mambo yake ya bila ya kushurutishwa na matakwa yao.Mnafiki anabakia kuwa mnafiki na mifano ipo hai imejaa tele. Hakuna asiejua yakuwa Misri walifanya uchaguzi halali kabisa na raisi akapatikana mchana mweupe halali kabisa mia kwa mia lakini akapinduliwa na mpaka hivi tunavyozungumza kuiongozi huyo halali yupo gerezani bila ya kufunguliwa mashitaka. Na hao wanaolalama kuhusiana na uchaguzi wetu mdogo wa ndani ndio marafiki namba moja wa nchi ya mbabe yule aliemsweka ndani raisi aliechaguliwa kihalali kule Misri. Dunia imekuwa kijiji hivi sasa na watanzania lazima tuamke tusije kurejea makosa ya wahenga. Waswahili wanasema mti wenye matunda ndio watu siku zote huutupia macho na Tanzania siku hadi siku zinavyokwenda mbele chini ya Magufuli imezifanya nchi nyingi duniani kuishangaa jinsi ianvyopiga hatua. Kuna nchi nyingi hasa zile za kibepari zingetamani sana nchi kama Tanzania iwe chini himaya zai kisiasa na kwa kuwazibiti viongozi wa nchi kwakufuata maelekezo yao lakini tatizo linakuja na wanakereka sana jinsi Magufuli pale anapokataa kuwa miongoni mwa wutumishi wao. Haijawahi kutokea tangu Afrika iumbwe katika zama hizi za mataifa huru ya Afrika, Raisi wa nchi ya Afrika kuchukua miaka mitatu kutosafiri kwenda ulaya au Marekani tangu awe raisi, awe raisi halali au wa kupindua kutosafiri kwenda ulaya . Magufuli amekataa mialiko yao mingi yaani ni matusi makubwa kwao. Kwanza wanajua kabisa kiongozi wa kiafrica na nchi zilizoendelea ni sawa na kidonda na nzi. Na kuwatumia nguvu yao ya misaada wanajua lazima wamtie kitanzi kiongozi wa kiafrica sasa anachokifanya Magufuli kwao ni ukosefu wa adabu na sawa ya kumuadabisha ni kama suala uhai na mauti na bado tutashuhudia mizengwe mingi labda Magufuli aachane na azima yake ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ianyojitegemea kiuchumi na kisiasa bila ya kufuata masharti ya nchi yeyote ile duniani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic