August 6, 2018


Kikosi cha Asante Kotoko kutoka Ghana kinawasili kesho jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza na Simba Jumatano ya wiki hii.

Timu hiyo kongwe kutoka Ghana itawasili Jumanne tayari kukipiga na wekundu wa Msimbazi katika tamasha la Simba Day ambalo hufanyika kila mwaka inapofikia Agosti 8.

Kotoko ambao wapo nafasi ya 4 katika msimamo wa Ligi Kuu Ghana wakiwa na tofauti ya alama 3 dhidi ya Ashanti Gold iliyo kwenye nafasi ya kwanza huku kila timu ikicheza mechi 15, wamekubali mwaliko wa kuja nchini.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari Simba, Haji Manara, amesema Kotoko watakuja na kikosi chao kamili tayari kuwapa upinzani mkali Simba katika mechi hiyo.

Wakati Kotoko wakiwasili kesho, kikosi cha Simba kinawasili leo nchini baada ya kumaliza kambi ya wiki mbili ambayo walikuwa wameweka Instabul, Uturuki.

3 COMMENTS:

  1. Hawa waghana wanaonekana wapo wagumu sana kimwili hata katika picha yaani ngangari. Sidhani kama mazoezi ya wiki mbili ya Simba yatatosha kuwapatia ushindi jumatano.

    ReplyDelete
  2. Mimi mawazo yangu naona msaada mkubwa Simba inayoweza kuwapa watani wake badala ya pesa cash kama ilivoombewa ni nayo kupewa fursa Asante Kotoko kujipima nguvu. Zopo faida mbili kubwa, nazo kujipima nguvu pia kipato kikubwa cha kiingilio ambcho kitakuwa cha halali cha kujitowa jasho kuliko kugaiwa hela jambo ambalo la aibu na kudhalilisha kutokana na heba kubwa ya yanga

    ReplyDelete
  3. Wazo zuri lakini kuna wachezaji wa yanga bado wamegoma na hata wale wanaoendea na timu bado wana donge rohoni linalowapelekea kufanya kazi kinyonge. Mtaalam mpya wa Simba aliekabidhiwa timu hivi majuzi anasema furaha kwa mchezaji ndio kila kitu kinachopelekea kuona kiwango halisi cha mchezaji. Na amejiapiza kuhakikisha kuwa wachezaji wake wanafanya kazi katika mazingira ya furaha sasa kutokana na hali ya yanga ilivyo hivi sasa kuirejesha furaha kwa wachezaji wake ni sawa na kumlazimisha paka kukutagia mayai. Yanga wanahitaji kuwaondoa wachezaji wote waliokuwa waajiriwa chini ya Yusufu Manji na kuleta vijana wapya watakaokubaliana na hali halisi ya sasa ya akina ndanda au mbao lakini bado wanajitolea kwa timu na kujituma kweli kweli.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic