August 6, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba unatarajia kutambulisha jezi zake mpya leo majira ya saa 5 asubuhi zitazotumika kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, amesema watatmbulisha jezi hizo maalum kwa ligi ambazo zitakuwa za nyumbani na ugenini.

Manara amesema wameamua kufanya maamuzi ya kutambulisha jezi hizo kuelekea Simba Day ili kuwafanya mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuzinunua kwa wingi ili waweze kwenda nazo Uwanjani Jumatano ya wiki hii.

Katika tamasha hilo ambalo hufanyika Agsoti 8 kila mwaka, Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana kwa ajili ya kukitambulisha rasmi kikosi chake kipya.

2 COMMENTS:

  1. Kuna usemi unaosema abebwae hujikaza na wakati mzuri na muafaka wa save pesa ni ule wakati wa neema hiyo ya pesa inapotokezea kupatikana kwa uhakika. Dunia hii ina mifano mingi sisi kama watanzania tunatakiwa kujifunza ili kupiga hatua zaidi za kimaendeleo. Tuliwashuhudia Wajapani baada ya timu yao ya taifa kutolewa katika mashindano ya kombe la Dunia kule Urusi, licha ya machungu ya timu yao kutupwa nje ya mashindano lakini baada ya mchezo kwisha na watu kaondoka uwanjani na kuacha kila aina ya uchafu kwenye seats wao wajapani walibakia uwanjani na kuanza kufanya usafi. Kitendo kile walikifanya ugenini sijui kwao watafanya nini? Mfano mwengine ni jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyodhibiti mapato na kuweza kuharamia miradi na huduma nyingi muhimu ambayo kwa akili zetu za kawadia za watanzania miradi hii yote inayogharamiwa na pesa za ndani hivi sasa ilipaswa kuombewa misaada kutoka kwa wafadhili wa nje? Nimenza na mifano hiyo yote madhumuni yangu ni kuwaambia wanasimba popote pale walipo nchini na nje ya nchi kuwa ni wakati muafaka wa kuiunga mkono timu kwa hali na mali hakuna haja ya kusubiri yaliowafika yanga ndio muanze kutembeza bakuli. Piga ua hakikisha unaiunga mkono klabu kwa kununua jezi ya timu. Hakikisha kama hujawa mwanachama wa kadi basi unapata kadi yako haraka na unalipa ada kwa stahiki yake, hakikisha uanahudhuria mechi na kama kuna uwezekano wa kubeba family yako basi unafanya hivyo ni moja ya kuleta uchangamfu kwenye family vile vile. Ada ya uanachama kwa timu ndio moyo wa timu katika ukasanyaji wa mapato ya timu. Simba tayari inammiliki mwenye hisa yakuwa moja ya wamiliki halali wa klabu lakini ndipo pale tunaposema abebwae hujishika sio kujiachia kabisa kabisa kwani hata Chelsea wanammiliki wa timu miongoni mwa matajiri wakubwa Duniani lakini bado wanachama na wapenzi wanajitolea kw nguvu zao zote kumuunga mkono tajiri wao na Mo anapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote ili kuweka mazingira mazuri ya ustawi wa timu. Kuhusu usimamizi wa mapato katika klabu zetu hasa Yanga kwa hivi sasa inaonekana viongozi wao bado akili zao zimeozea katika enzi za upigaji na kujisahau kabisa misili ya mwizi aliejificha kwenye kichaka cha njugu wakati mwili wote unaonekana. Mapato yanayoingizwa na taasisi kadhaa za serikali na kugharamia miradi mikubwa ya ajabu ni ushahidi tosha pale Yanga pana uozo mkubwa si wa kulia njaa wala si wa kukosa mfadhili. Serikali inapaswa kupeleka wachunguzi wake wa mapato na mahesabu kujua kulikoni pale yanga? Timu lazima ziwe na wabunifu na watu wa kujitolea kwa ajili ya klabu sio blah blah tu. Na kwa maelezo ya mzee akili mali katika mahojiano aliyoyafanya katika vituo mbali mbali vya television hivi karibuni amethibitisha yakuwa Yanga kuna wapigaji wa nguvu na walimpiga Yusufu Manji vibaya vibaya hadi kuunda makundi feki kwa ajili yakwenda kukutana nae ili wapige pesa ya vikao na watu hao bado wapo pale yanga na ndio wanaoimaliza timu hivi sasa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli kabisa lakini za mwizi ni arobaini ngoja tubezwe kwa ajili yao mwisho wao umefika.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic