August 16, 2018


Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetangaza marefa watakaochezesha mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar.

Waamuzi hao ni Refa wa kati ambaye ni Elly Sasi wa Dar es Salaam, Msaidizi namba 1 ni Ferdinand Chacha wa Mwanza huku wa pili ni Helen Mduma wa Dar es Salaam, Fouth Official ni Jonesia Rukya kutoka Bukoba.

Match Assessor ni Alfred Rwiza wa Mwanza na Match Commissioner ni Said Sudi wa Tanga.

Mchezo huo ambao utachezwa siku ya Jumamosi ya Agosti 18 katika dimba la CCM Kirumba, Mwanza viingilio vyake tayari vimeshatajwa ambavyo ni 10000 kwa VIP, 5000 kwa Mzunguko na Watoto ni 1000.

Simba watashuka dimbani wakiwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara huku Mtibwa wakiwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic