EXCLUSIVE: MDHAMINI MKUU LIGI KUU BARA KUTANGAZWA
Na George Mganga
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura amesema Ligi Kuu msimu wa 2018/2019 itaanza bila ya mdhamini Mkuu ambaye atatangazwa baada ya Ligi kuanza.
Wambura amesema Mdhamini huyo atatangazwa kwa baadaye ili kuendana na ratiba ya Ligi Kuu iliyotangazwa kuanza Agosti 22 2018.
Mpaka sasa Ligi Kuu Bara ina wadhamini wawili pekee ambao ni Azam Pay Tv pamoja na Bank ya KCB ambayo imeingia mkataba wa kudhamini Ligi Kuu Bara ikitoa kiasi cha fedha milioni 420.
Inaonekana dhahiri shahiri Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom iliyokuwa ikidhamini ligi kwa muda mrefu imeshindwa kufikia mwafaka wa kuongeza mkataba mwingine na TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment