August 15, 2018




DStv sasa kurusha Serie A-  kifurushi cha Bomba!
·         Mechi zote 380 kwenye ‘live’ HD ndani ya Bomba
·         Pia Mechi zote 380 za La Liga kuonekana
·         Mechi 108 za Ligi ya Uingereza (EPL) nzao ndani ya Kifurushi cha Bomba

Siku chache tu kabla ya kuanza kwa moja ya ligi maarufu Duniani – Ligi kuu ya Italia Serie A, MultiChoice imetangaza neema ya burudani kwa wateja wake kwa kuweka michezo yote 380 ya ligi hiyo katika kifurushi cha chini kabisa cha DStv Bomba ambacho hulipiwa shilling 19,000 tu kwa mwezi.

Kama hiyo haitoshi, DStv pia itaonyesha mechi zote 380 za ligi ya Hispania – La Liga katika kifurushi hicho cha bomba huku mechi 108 za ligi kuu ya uingereza (EPL) nazo zikionyeshwa katika kifurushi hicho cha chini kabisa.

“Kama ilivyo ada, sisi DStv kila uchao tunahakikisha kuwa tunamfikishia mtanzania burudani popote alipo na kwa gharama nafuu. Hii ndiyo sababu tumeamua kuiweka ligi hii maarufu katika kifurushi chetu cha Bomba kinachopatikana kwa shilingi 19,000 tu kwa mwezi” amekaririwa Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria.

“Tunatambua kuwa ligi ya Italia ni moja ya ligi zenye mvuto mkubwa ulimwenguni na kama kawaida kwa kupitia DStv, tunawafanya watanzania kuwa sehemu ya ulimwengu wa burudani hususan soka, hivyo tumeamua kwa makusudi kabisa kuiweka ligi hii ya italia kwenye kifurushi cha bomba” amebainisha Alpha.



Wiki iliyopita DStv ilitangaza kuirejesha ligi hiyo ya Italia na kuweka michezo michache kwenye kifurushi cha Bomba, lakini kutokana na maoni ya wateja wake wengi, imeamua kuishusha ligi hiyo katika kifurushi cha chini kabisa.


Ligi Kuu ya Italia inatarajiwa kuanza Jumamosi hii ambapo washabiki wa soka watamshuhudia mwanasoka nguli Christiano Ronaldo akiiwakilisha timu maarufu ya Juventus kwa mara ya kwanza. Mtanange huo wa ufunguzi utakuwa kati ya Juventus na Chievo na utaonyeshwa mubashara kupitia DStv chanel ya SuperSport 8 (HD).


Mbali na hayo, wateja wa DStv wataendelea kufurahia  msimu huu mpya wa soka na katika kunogesha zaidi michuano ya ligi ya uingereza itatangazwa kwa lugha ya kiswahili.


Ili kuwapa wateja wake uhuru zaidi wa kufurahia soka popote walipo,  DStv inaendelea kutoa huduma ya DStv Now ambapo mteja wa DStv anaweza kutazama matangazo katika vifaa zaidi ya vinne kama vile simu, kompyuta, na televisheni ya kawaida.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic