Muigizaji mkongwe nchini Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka kuwa raha yake kubwa siku zote ni kuona Simba inamfunga Yanga na si kitu kingine.
JB alisema hayo ikiwa ni siku chache kuelekea siku maalum ya Simba Day ambayo itafanyika Jumatano ya Agosti 8, mwaka huu lengo likiwa ni kutambulisha wachezaji wao wapya ndani ya Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Spoti Xtra, JB alisema; “Najua tunaenda kwenye siku maalum ya Simba Day na safari hii watu wajue kuwa tuna timu sio ya kubabaisha lakini pamoja na hayo mimi raha yangu ni kuona nafanikiwa kuifunga Yanga ni kitu ambacho nakipenda na safari lazima iwe hivyo.”
“Nakuwa na kiburi hiki kutokana na usajili ambao tumefanya safari hii yaani hata kocha mwenyewe anachanganyikiwa ni jinsi gani ataweza kupanga timu yake sababu kikitoka kitu kinaingia kitu hivyo Yanga wajipange tu,” alisema JB.
0 COMMENTS:
Post a Comment