August 8, 2018


Macho yakizoea kuona kitu fulani halafu ghafla kikapotea; siku kikionekana viungo hivyo vya kutazamia hukifanya kuwa maalum; kilichomtokea mrembo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo hivi karibuni alipogandana na mtu mwenye asili ya Kiasia kinathibitisha hili, acha Risasi likupashe.

Jokate aliyekuwa siku za nyuma akijichanganya katika ishu nyingi na kuonekana mara kadhaa kwenye vyombo vya habari na baadaye kujiweka mafichoni, alipoibuka kwenye arobaini ya mtoto wa Zamaradi Mketema iliyofanyika Jumatano wiki hii Mabwepande, jijini Dar; macho ya wengi yalikodoka kwake na  kuzua maswali lukuki. “Amebadilika.” “Amependeza hata nguo aliyovaa imemkaa kweli.”“Lakini siku hizi ana ishu gani mbona kama kapoa sana?”

“Huyu dada anajitambua tofauti na baadhi ya mastaa wengine wa kike, si bure kuna kitu kimembadilisha,” maneno machache kutoka kwa baadhi ya waalikwa wa shughuli hiyo ambayo Risasi liliyanasa katika pitapita zake kwenye arobaini hiyo ya mtoto. Baada ya viulizo vingi kujitokeza juu ya mrembo huyo, funga kazi ikawa ni pale alipogandana na mtu mwenye asili ya Kiasia ‘Mdosi’ ambaye hakukuwa na utambulisho wake kabla ya tukio hilo.

“Huyo ndiyo jamaa yake nini?” msanii mmoja maarufu wa Bongo Muvi (jina kapuni kwa sababu Risasi halikumwandaa kihabari) alimuuliza mwalikwa mwingine. Ingawa hakukuwa na dokezo za wazi la wawili hao kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi lakini maswali ya wengi yalitaka kujua mdosi huyo ni nani yake Jokate pengine kwa jinsi walivyokuwa wakizungumza huku wakiwa wamekaribiana ziro ‘distensi’.

Hata hivyo baadaye Risasi lilitokezwa kuwa Mdosi huyo ni rafiki wa wafanyakazi wa Kampuni ya Happix ambayo ilikuwa imedhamini shughuli ya arobaini hiyo na kwamba ukaribu wa wawili hao lilikuwa ni jambo lisilofahamika na wengi. Kuhusu kutoonekana kwa mrembo huyo kwenye baadhi ya matukio na kusitisha maisha ya ‘kujirusha’ mmoja wa watu wa karibu naye aliliambia Risasi kuwa: “Huo ni utu uzima.” Ulitaka aendelee kuishi kitoto.”

Jokate ni Miss Tanzania namba 3, 2006, mwanamitindo, mjasiriamali na anatajwa kuwa ni mpenzi wa zamani wa Ali Kiba na Hasheem Thabeet.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic