August 27, 2018


Na George Mganga

Dakika 90 zimelizika kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa timu ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mabao pekee ya mchezo huo yamewekwa kimiani na straika hatari aliyesajiliwa kutoka Gor Mahia FC katika dakika za 11 na 45+3.

Baada ya kuingia kambani mara mbili, Kagere amefikisha jumla ya mabao matatu ndani ya mechi mbili baada ya kufunga kwenye mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons ambao Simba ilishinda 1-0.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya alama 6 ikishinda mechi zote ambapo Mbeya City bado haina alama zozote mpaka sasa kutokana na kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Azam FC.

Wekundu hao wa Msimbazi kwa mujibu wa ratiba ya ligi, inaonesha kuelekea mchezo ujao watakuwa wanacheza dhidi ya Lupuli FC ya Iringa katika Uwanja wa Taifa Dar.

1 COMMENTS:

  1. Well done Simba well done Kagere. Bado John Bocco hayupo kwenye kiwango chake lakini tunaamini utafunga magoli na Kagere na Okwi na Kichuya na HD Dilunga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic