August 17, 2018


Na George Mganga

Wakati kesho ikisubiriwa kwa hamu na wadau wa soka jijini Mwanza pamoja na pande zingine hapa nchini kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Hisani ambapo Simba na Mtibwa watakutana kuiwania kesho, Katibu wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, amewapa ubingwa Mtibwa.

Licha ya kuweka kambi ya wiki mbili huko Instabul, Uturuki, Akilimali amesema hakuna chochote cha maana ambacho Simba wameambulia na badala yake kesho wategemee ushindani mkubwa kutoka kwa Mtibwa.




Akilimali amesema kwa namna kikosi cha Mtibwa kilivyo ana uhakika kitawaweza kuwashangaza wengi kwenye mechi hiyo ambayo Simba inapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Katibu huyo amesema kambi ya Simba Uturuki haitakuwa na kipya bali imekuwa ikikuzwa na vyombo vya habari pekee kwa kuipaisha kuwa itaonesha maajabu.

"Mimi naimani kabisa Mtibwa wataonesha maajabu mbele ya Simba kesho, hakuna cha maana walichokipata Uturuki na hilo ndiyo litathibitika kesho. Timu imekuwa ikipaishwa na vyombo vya habari na haina chochote kipya, ni kama zamani tu" alisema.

Simba na Mtibwa zinashuka kesho kuwania ngao hiyo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambapo mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni na itarushwa LIVE kupitia AZAM TV.

4 COMMENTS:

  1. Huyo Akilimali anacheo gani Yanga na yeye ndio amekuwa msemaji wa Mtibwa

    ReplyDelete
  2. Hivi mlitegemea aseme kuipa ushindi Simba?

    ReplyDelete
  3. Mzee akilimani Pambana na Hali yako njaa itawauwa wachezaji wako Mzee kushindia matikiti Maji duuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic