SIMBA KUKIPIGA NA WAARABU LEO
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kushuka uwanjani leo Jumamosi majira ya kumi alasiri kukipiga dhidi ya mabingwa wa sasa wa Ligi Kuu ya Morocco, Ettihad Riadi De Tanger.
Timu hizo zitacheza mchezo huo wa kirafiki nchini Uturuki ambapo zote zimeweka kambi nchini humo kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao wa 2018/19.
Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni muhimu kwa timu zote kwa kuwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya na utakuwa na faida kwa pande zote mbili.
IR Tanger walitwaa ubingwa wa msimu uliopita wakifuatiwa na Wydad Casablanca huku DifaĆ¢ El Jadidi ambayo Mtanzania, Simon Msuva anaichezea ikimaliza ligi kwa kushika nafasi ya tano.
Akizungumzia michezo hiyo ya kirafiki Aussems alisema: “Kwangu mimi na benchi la ufundi ni sehemu ya mazoezi lakini wachezaji watacheza kama mechi na wanatakiwa kufurahia. Tumekuwa tukifanya mazoezi mara mbili kwa siku, hiyo itatusaidia kujua mambo kadhaa ya kimbinu.”
Awali, juzi Simba ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Moulodia Oudja ya Morocco uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika kiwanja cha Hoteli ya The Green Park kilichopo katika mji mdogo wa Kartepe, Kocael.
Bao la Oujda lilifungwa dakika ya 55, la Simba lilifungwa na Adam Salamba dakika ya 58 huku mchezo ukimalizika dakika ya 65 kutokana na mvua kubwa.
Simba inashuka kikipiga na Waarabu hao ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Morocco baada ya mchezo huo jana kuahirishwa sababu ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha huko Instanbul.
Kila la kheyr Mabingwa wa Tanzania
ReplyDeleteNi kipimo kizuri sana kukipiga timu kama hiyo ambayo kati ya timu bora kabisa za Africa sasa club bingwa ya Moroco na kuwahi kuchukuwa ubingwa wa Africa. Ni vizuri kukumbana na timu yenye uwezi mkubwa kuliko vitimu visivokuwa na uwezo wowote. Tunaitakia Simba kila la kheri
ReplyDelete