Licha ya kuwa na wakati mgumu ikiwemo kuyumba kwa uchumi, klabu ya Yanga imemwaga msaada wa mipira mitatu kwa timu ya Mkamba Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.
Msaada huo umekabidhiwa na viongozi wa Yanga kwa Mkamba baada ya kucheza mchezo wa kirafiki na kuweza kushinda bao 1-0 likiwekwa kimiani na Papy Tshishimbi.
Yanga imewapa Mkamba mipira hiyo kwa lengo na madhumuni la kuwasaidia kwa ajili ya kufanyia mazoezi ili kupigania nafasi ya kupanda daraja la kwanza.
Kikosi hicho sasa baada ya kucheza na Mkamba kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea Dar es Salaam kuanzia leo tayari kukipiga na USM Alger.
Yanga itacheza na waarabu hao katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0 huko Algiers, Algeria.
Hivi mipira mitatu ndiyo msaada wa maana kweli?
ReplyDelete