Ajenti wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba anatarajiwa kuwaambia Red Devils kuwa anaweza kufikia makubaliano ya pauni milioni 100 kwa mshindi huyo wa kombe la dunia mwenye umri wa miaka 25 kwenda Barcelona. (Daily Star Sunday)
Pia meneja wa Manchester United Jose Mourinho anapanga kuweka siku ya mwisho kumwinda mlinzi wa England Harry Maguire, 25, ambaye amewekewa thamani ya pauni milioni 80 na Leicester. (Sunday Express)
Manchester United wanakaribia kuafikia makubaliano ya paunia milioni 60 kumsaini mlinzi wa Tottenham Toby Alderweireld, 29. (Sunday Mirror)
Lakini mbio za Manchester United za pauni milioni 35 kwa mlinzi wa Barcelona raia wa Colombia Yerry Mina zimefikia kikomo kwa sababu ya mvutano kuhusu malipo ya ajenti. (Sun on Sunday)
Chelsea wanaweka tayari pauni milioni 35 kwa kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27. (Sunday Express)
Chelsea watafanya mazungumzona mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard siku ya Jumamosi na kumpa mchezaji huyo wa miak 27 mkataba kwa pauni 300,000 kwa wiki kumzuia asijiunge na Real Madrid. (Sunday Times - subscription required)
Manchester United watamtoa mshambuliaji mfaransa Anthony Martial, 22, kwa Chelsea kumbadilisha na wing'a Mbrazil Willian, 29, huku wachezaji hoa wakiwekewa thamani ya pauni milioni 75. (Sunday Mirror)
Borussia Dortmund wanakataa kumuuza wing'a mmarekani anayewekewa thamani ya pauni milioni 60 Christian Pulisic, 19, anayetafutwa pia na Chlsea na Bayern Munich. (Mail on Sunday)
Wolves wametoa ofa ya pauni milioni 16 kwa mlinzi wa Besiktas na Croatia Domagoj Vida, 29. (Sabah - in Turkish)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment