TIMU NNE ZAMUITA MSUVA ULAYA, JADIDA WATAKA BILIONI NNE
Timu nne kutoka nchi za Ulaya zimeonyesha nia ya wazi kumuwania mshambuliaji wa Klabu ya Difaa El Jadida, Simon Msuva anayekipiga katika Ligi Kuu ya Morocco.
Msuva alijiunga na El Jadida, Julai 29, mwaka jana kwa dau la dola 150,000, sawa na zaidi ya Sh milioni 337 akitokea Yanga ambapo amefanikiwa kuonyesha kiwango kiasi cha kuzishawishi timu nyingine hasa zile za Ulaya.
Tangu atue klabuni hapo Msuva amekuwa mchezaji pekee wa kigeni katika timu hiyo aliyetoa msaada mkubwa kwa kuifungia mabao mengi kuanzia kwenye ligi kuu hadi Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo kusababisha kuongezeka thamani yake.
Kwa mujibu wa Championi, baba mzazi wa Msuva, mzee Happygod Msuva alisema kuwa, kwa sasa mwanaye huyo anafuatiliwa na timu nne zikiwemo za Ulaya na nyingine nchini humo kwa kuhitaji huduma yake lakini dau la El Jadida limekuwa likiwakwamisha.
“Kuna timu anaendelea kufanya nazo mazungumzo ambazo zimemfuata Msuva ndani ya Morocco na nje ya Morocco ikiwemo timu kutoka Hispania ili kuweza kumsainisha lakini tatizo kubwa limekuwa kwa klabu yake, lakini siwezi kuziweka wazi hizo timu hadi mipango itakapokamilika.
“Al Jadida inahitaji karibu shilingi bilioni 4 za Kitanzania dau ambalo ni kubwa hivyo anaendelea na mazungumzo na iwapo atafanikiwa basi anaweza kuondoka wakati wowote kwani ndiyo matarajio yake,” alisema mzee Msuva.
Kama kawaida, angekuwa yupo Tz, ungesikia mnambania mwacheni aende , tujifunze soka biashara.
ReplyDeleteMpira kweli ni biashara nakuunga mkono Philemoni Kalomo wabongo tunapenda sifa kuuza mchezaji nje ya nchi hata kama anauzwa kwa hasara kuna baadhi ya timu zikikuwa hazitaki kuuza mchezaji wao Tegemeo kwa bei ndogo zikasakamwa kuwa zinabania wachezaji mfano ndo huo tujifunzeni kwa wenzetu Chelsea wenyewe wameweka dau kubwa kwa madrid ili kumnasa Hazard ila ingekuwa bongo ingekiluwa skendo
ReplyDeleteAcha kulingalinisha Chelsea na Yanga au Simba. Iko hivi Mpaka sasa Tanzania inawachezaji wachache sana nje ikilinganishwa na wenzetu Uganda achilia mbali Congo. Tatizo nikwamba mawakala wanapowaona wachezaji wakiwa Yanga au Simba mnake ndio zinabadilishana kucheza Klabu bingwa Afrika, huwa hawaamini viwango vya wachezaji kutokana na Klabu zenyewe kutokuwa na mafanikio kwenye mashindano ya Afrika, pamoja na kiwango cha soka la nchi yetu. Sasa Msuva alikuwa mzuri tangu akiwa yanga, lakini Diffa walitoa kiduchu kulingana na wasiwasi kwamba ataweza? Sasa Yanga wangekataa bei ile kweli wangekuwa wamemlostisha yeye. Unataka mchezaji atokee Tanzania aende ulaya timu kubwa, wakala gani atakuwa mwehu kucheza bahati nasibu ya hivyo? Hata hivyo Diffa usiwafananishe na Yanga, hata kiwango cha Morocco sio cha kulingana na Tanzania. Mchezaji akingara ligi ya kule lazima wazungu waje, manake wanajua viwango vya nchi za Africa kaskazini na Magharibi, kwani wamefanya nao biashara ya wachezaji muda mrefu tu. Tatizo lenu kidogo, matoa mifano ya Chelsea, ManU, nk. Kinganisheni kwanza na ukanda wa Afrika kabla ya kwenda ng'ambo.
DeleteKwanza tufahamu nafasi yetu kama nchi, halafu tujilinganishe na wenzetu. Kijiografia Moroco IPO Afrika lakini Kibiashara IPO Ulaya. Ni rahisi zaidi mchezaji kuuoneka akiwa huko kuliko akiwa hapa kwetu. Unamng'ang'ani hapa bongo kwa sh. Ngapi? Chelsea wanamng'ang'ania Hazard wana Vingi vya kumpa, wanaweza kupata ubingwa hata wa Ulaya na pesa nayo ipo ya kuridhisha.sasa sisi tunamng'ang'ania ili tumpe mini? Hapa tujifunze namna ya kutengeneza mikataba ambayo itasaidia timu hata kama mchezaji akindelea kuuzwa huko mbele.
ReplyDeleteUmesema Kyando, Sisi Bado hatutakiwi Kuwanyima fulsa vijana .
ReplyDeleteWapo wengi walinyimwa fursa na Leo tupo nao mtaani hakuna wa kumsaidia mwenzake, iliyobaki tunachekana ujinga!
ReplyDelete