POGBA SASA KUONDOKA MANCHESTER
Mwanasoka Mfaransa, Paul Pogba anataka kuondoka Manchester United ya Uingereza na kwenda Barcelona ya Hispania hata kama ugomvi wake na kocha/meneja wake, Jose Mourinho ukimalizika.
Ili kumpoza mchezaji huyo, Mourinho alimpa ukapteni katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Leicester, hata hivyo, alipoulizwa baada ya mechi alijisikiaje, Pogba alisema asingeweza kujibu chochote kwa kuogopa kwamba angepigwa faini na klabu hiyo.
“Kuna mambo nikiyasema, klabu itaniadhibu kwa kunipiga faini,” alisema.
Imeonekana kwamba lengo kuu la mchezaji huyo ni kuichezea Barcelona, hilo la ugomvi wake na Mourinho ni la pili.
Pogba, 25, aliyendoka Man U wakati wa kocha Sir Alex Ferguson na kwenda Juventus mwaka 2012, amemwambia naibu mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo, Ed Woodward na wasaidizi wake kwamba anataka kuondoka.
0 COMMENTS:
Post a Comment