August 16, 2018


Na George Mganga

Hatua ya marekebisho ya Uwanja wa CCM Kirumba uliopo Mwanza yanaendelea vizuri kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Hisani.

Uwanja unaelekea hatua ya mwisho kwa ajili ya kuzikaribisha Simba na Mtibwa ambazo Agosti 18 2018 zitakuwa zinawania Ngao ya Hisani.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) liliamua kuupeleka mchezo huo Mwanza ili kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wa huko sababu ni moja ya mikoa iliyopo Tanzania.

Simba ambao wapo Arusha baada ya kucheza na Arusha United katika mchezo wa kirafiki jana, wanatarajiwa kuwasili muda wowote Mwanza tayari kukipiga na Mtibwa.

Mtibwa wanaenda kucheza na Simba wakiwa mabingwa wa FA huku Simba wakifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2017/18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic