August 21, 2018


Paris St-Germain ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Croatia Ivan Rakitic lakini Barcelona haiko tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye miaka 30 ambaye kipengee cha kumuuza ni cha thamani ya Euro 125m (£112.2m). (Marca)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Real Madrid Luka Modric, mwenye umri wa miaka 32, amesema tuhuma kuwa amewasiliana na Inter Milan kuhusu uhamisho wake katika msimu wa joto kama "upuuzi mkubwa kihistoria". (Mirror)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City raia wa Ukrain Oleksandr Zinchenko, aliye na miaka 21, anatarajiwa kujiunga na timu ya Uhispania Real Betis kwa mkopo wa msimu mzima.(Sun)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, mwenye umri wa miaka 22, huenda akaelekea Uhispania kwa mkopo baada ya kutemwa katika kikosi cha Maurizio Sarri kitakachokabiliana na Arsenal mwishoni mwa juma. (Mirror)

Hatahivyo, Chelsea inamtaka Loftus-Cheek asalie na aipiginie nafasi yake licha ya mchezaji huyo kuudhika na hatua hiyo ya kutemwa katika kikosi.(Telegraph)

Middlesbrough inakaribia kufikia makubaliano ya wachezaji wawili wa Everton raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Yannick Bolasie, aliye na miaka 29, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Serbia Muhamed Besic, mwenye miaka 25. (Star)

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry, mwenye miaka 41, ana hamu ya kuchukuwa usukani wa timu ya Ufaransa Bordeaux, anasema aliyekuwa meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger. (Corse Matin - in French)

Kutoka BBC

1 COMMENTS:

  1. Jamani kuweni makini na taarifa za kukopi na kupaste, hivi hii taarifa ni ya lini? Tazama mlivyobugi au kuna mchezo mwingine wikendi hii kati ya arsenal na chelse?

    (Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, mwenye umri wa miaka 22, huenda akaelekea Uhispania kwa mkopo baada ya kutemwa katika kikosi cha Maurizio Sarri kitakachokabiliana na Arsenal mwishoni mwa juma. (Mirror))

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic