August 17, 2018


Na George Mganga

Baada ya Simba kutikisa katika tamasha lao kubwa la Simba Day Agosti 8 2018, uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting umesema unakuja kitofauti zaidi ili kuwapoteza wakongwe hao.

Msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire, ameeleza kuwa kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaoanza Agosti 22, watahakikisha wanaujaza Uwanja nje na ndani ili kuwazidi kete Simba.

Bwire amesema kwa mipango na namna kwa ujumla walivyojipanga kuelekea msimu mpya, wanaimani watawapoteza Simba pamoja na Yanga kwa kuingiza watu Uwanjani pamoja na kuwapa soka la kifundi.

""Unajua hawa Simba wanatamba kuwa waliujaza Uwanja wa Taifa, sasa ninawaambia Watanzania kuwa msimu ujao kuna jambo kubwa tumeliandaa, tunataka kuujaza Uwanja wa Taifa nje na ndani kuwazidi wao ili kuonesha dhahiri kuwa tunakuja na staili mpya ya mpapaso square ambayo tumeifanyia maboresho" alisema.

Msemaji huyo mwenye mwembwe nyingi nchini ameahidi Ruvu Shooting kuja na mfumo wa kitofauti unaojulikana kwa jina la MPAPASO SQUARE utakaokuwa na matokeo chanya pekee kwao.

Jeuri hiyo imekuja kutokana na maandalizi ambayo Ruvu Shooting imeyefanya ambayo Bwire anaamini kuboreshwa kwa mfumo wa MPAPASO SQUARE utawafanya wengi kulala na viatu ikiwemo Simba na Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic