August 17, 2018


Na George Mganga

MABINGWA wa kihistoria katika soka la Tanzania kwenye Ligi Kuu Bara, Young Africans wakiwa na rekodi ya kuutwaa kwa mara 27, wanarejea leo jijini Dar es Salaam tayari kukamilisha maandalizi dhidi ya USM Alger.

Yanga walikuwa kambini Morogoro kwa wiki mbili ambapo walicheza michezo mitatu ya kirafiki dhidi ya Tanzanite Academy, Mawenzi Market na Mkamba Rangers FC.

Baada ya kambi hiyo kumalizika, Yanga sasa inarejea nyumbani kukamilisha maandalizi ya kukipiga na USM Alger katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Agosti 19 2018.

Wababe hao wa soka la Tanzania wamekamilisha kambi yao Morogoro ambayo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Jumapili dhidi ya Waarabu huku pia wakiweza kumuaga Nadir haroub 'Cannavaro' kwa mechi maalum na Mawenzi ambayo walishinda 1-0.

Wakati zikiwa zimesalia siku mbili pekee kucheza na Alger, Yanga wamesema watautumia pia mchezo huo wa Kombe la Shirikisho ili kumuaga aliyekuwa beki wake Cannavaro ambaye ametundika daruga la kucheza soka la ushindani.

Cannavaro ambaye ameichezea kwa mafanikio makubwa Yanga pamoja na Taifa Stars atapata fursa ya kuagwa na wakazi wa Dar es Salaam Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

1 COMMENTS:

  1. KAGAWA DOZI KWA TEAM ZIPI....WABONGO BANA HAPO NI SAWA NA KUKARIRI ORODHA ALAFU UNASEMA UPO TAYARI KUFANYA MTIHANI WA FORM FOUR...HIVI KWELI YANGA KWA TEAM HIZO MLIZOCHEZA NAZO MPO TAYARI KUMKABILI MWARABU AU MNYAMA/AZAM..KWELI???AU NDO MNATAFUTA KUUWA WATU KWA PRESHA PALE TAIFA SIDHANI KAMA MTAKUWA SALAMA KWA MWARABU..JUMAPILI PUNGUFU 3..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic