August 16, 2018




Ukisema mambo safi utakuwa haujakosea baada ya timu ya taifa ya vijana ya chini ya miaka 17 kushinda kwa mabao 5-0 dhidi ya Sudan.

Serengeti Boys imeangusha kipigo hicho maridadi dhidi ya Sudan katika  michuano ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kwa ushindi huo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Serengeti Boys imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.


Ushindi huo mnono wa mabao matano, unaifanya Serengeti Boys ifikishe pointi sita baada ya mechi mbili na kupanda kileleni, Rwanda yenye pointi sita imeporomoka, huku Serengeti ikisaidiwa na wastani wao mzuri wa mabao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic