MAANDALIZI YA SIMBA NA MTIBWA KUKIPIGA CCM KIRUMBA YAKO TAYARI, KIZUGUTO AFUNGUKA
Na George Mganga
Afisa Mtendaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Baraka Kizuguto, amesema maandalizi ya kuelekea mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Simba na Mtibwa yamekamilika.
Kizuguto ameeleza kuwa tayari kila kitu kipo sawa kuelekea mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wengi wa soka jijini Mwanza na pande zingine hapa nchini.
Ikiwa imesalia siku moja pekee mechi hiyo kupigwa ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Kizuguto amesema tayari Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo wameshawasili Mwanza.
Wakati Kizuguto akizungumza hayo, kikosi cha Simba kinaondoka leo kuelekea jijini Mwanza kwa njia ya anga tayari kumalizana na Mtibwa.
Simba wanaenda kucheza mechi hiyo wakiwa wametoka kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Arusha United iliyo daraja la kwanza huko Arusha ambapo ilishinda kwa mabao 2-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment