Na George Mganga
Kaimu Rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah, aliwasili bandarini hapo na kuanza kuzikagua nyasi hizo ambazo muda wowote inalezwa zitasafirishwa kuelekea Bunju kwa ajili ya ujenzi.
Ikumbukwe awali nyasi hizo zilizuiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na kutolipiwa fedha baada za kuwasilishwa bandarini na Simba kulazimika kulipia kiasi cha shilingi milioni 80 za kitanzania.
Simba ilitumia shilingi milioni 80 kuzikomboa nyasi hizo kwa kile kilichoelezwa kukaa bandarini kwa siku 60 baada ya kuwasili na kusababisha kusimamisha ujenzi wa uwanja wao uliopo Bunju jijini Dar es Salaam.
Lakini baada ya klabu hiyo kubadili mfumo wa uendeshwaji ambapo sasa imepata mwekezaji tajiri na kijana bilionea Mohammed Dewji 'Mo', nyasi hizo sasa zitachukuliwa kupelekwa Bunju tayari kwa kutumika.
0 COMMENTS:
Post a Comment