August 21, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza rasmi viingilio vya mchezo wa kesho ambao utakuwa ni wa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19.

Simba wataanza rasmi safari ya kutetea ubingwa ambao wameutwaa msimu uliopita dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, amewamba mashabiki na wapenzi wa Simba kujitokeza kwa wingi ili kuipa hamasa timu yao ili iweze kupata matokeo chanya kwenye mechi hiyo.

Simba itaingia Uwanjani ikiwa na Kocha wake mpya, Mbelgiji, Patrick Aussems ambaye alichukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre ambaye alimaliza mkataba wake wa miezi mitano.

Viingilio vya mchezo huo ni kama ifuatavyo

VIP A 15,000 (ELFU KUMI NA TANO)
VIP B 10,000 (ELFU KUMI)
MZUNGUKO 3,000 (ELFU TATU)
WATOTO 1,500 (ELFU MOJA NA MIA TANO TU)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic