ALIKIBA NA MKEWE WAWASAIDIA YATIMA KIGAMBONI
Nguli wa Bongo Fleva, Alikiba mke wake Amina sambamba na watu wake wa karibu wamewatembelea watoto wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Amani Orphanage Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam na kuwaptia msaada wa vitu mbalimbali.
Staa huyo ametoa msaada huo zikiwa ni siku chache tangu aliporejea nchini akitokea Toronto nchini Marekani alipokwenda kufanya shoo ya Tamasha la Africa All Star Music Fest.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Kiba ameandika;
“Education, food, shelter, and, love that’s all they need from you ❤️ me and my lovely wife 🤪 we do #AmaniOrphanageFoundationKigamboni #KingKiba”.
0 COMMENTS:
Post a Comment