SIMBA YATOA SOMO ARUSHA
Na George Mganga
Baada ya mchezo wa kirafiki wa Simba dhidi ya Arusha United kumalizika kwa wekkundu wa Msimbazi kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema timu yake imetoa somo Arusha.
Makonda ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi wa mechi hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amefunguka kuwa kwa namna Simba walivyocheza watakuwa wamewafundisha vizuri Arusha United walio daraja la kwanza.
Kiongozi huyo ambaye ni shabiki mnazi wa Simba ameeleza kitendo cha Simba kucheza na timu hiyo ni jambo la kujifunza kwao sababu wamepata ushindani na kikosi ambacho kina wachezaji wakubwa na wenye uwezo.
Aidha, Makonda amesema baada ya Simba kurejea jijini Dar es Salaam, wapinzani wake wategemee kuoneshwa soka la kimataifa zaidi kulingana na usajili ambao klabu imeufanya.
Simba itarejea jijini Dar es Salaam mapema baada ya kucheza na Mtibwa Sugar Agosti 18 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Hisani.
0 COMMENTS:
Post a Comment