SINGIDA UNITED WAFUNGUKA JUU YA USHIKAJI WAO NA YANGA
Uongozi wa Singida umekanusha kwa asilimia 100 kuhusiana na taarifa ambazo zimekuwa zikielezwa kuwa ina ushikaji na Yanga.
Hatua hiyo imekuja kufuatia hivi karibuni Singida kuisaidia Yanga baadhi ya wachezaji ili waweze kuisaidia timu katika mashindano ya kimataifa na Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida, Festo Sanga, ameeleza kuwa wao na Yanga hawana ukaribu wowote ule ambao umepelekea klabu yao kuisaidia Yanga wachezaji.
Ukiachana na Sanga, Singida United kupitia Mlezi wake, Mwigulu Nchemba, aliweka wazi kuwasaidia Yanga na akasema yupo tayari kuwasaidia wengine ikiwemo Simba ili waweze kufika mbali kisoka.
Mwigulu alisema kuwa alikuwa anahojiwa kwanini anawapa msaada Yanga ndipo akaibuka na kueleza kwamba yeye ni mtu wa mpira na si Yanga pekee anaweza kusaidia bali hata timu zingine.
Abu kwa Kiongozi wetu Mwigulu kudanganya kuwa yeye anaweza kusaidia pia timu nyingine kama alivyofanya kwa Yanga lakini pia kuiingiza Singida United kwenye majaribio yasiyo ya kiushindani ndani ya soka. Aibu kusema uongo, Aibu kudanganya. Ni kukosa basics za uongozi bora.
ReplyDeletePia alisema anaisadia yanga kwa sababu yeye ni mwanachama wa yanga na hawezi kuwacha kuisaidia yanga ikiwa ipo kwenye matatizo...usikanushe kipuuzi ukadhani watu hatufuatilii vyombo husika hiyo kusema hata simba anaweza kuwasahidia kajikosha tu..kama unabisha check hii youtube :https://www.youtube.com/watch?v=Wa9rANSyNhA
Delete