TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 140 UBORA WA SOKA DUNIANI, UFARANSA YAONGOZA
Timu ya soka ya Wanaume ya Ufaransa imefanikiwa kushika namba moja katika orodha ya timu bora za Dunia iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka la Dunia(FIFA)
Ufaransa imefanikiwa kushika nafasi hiyo ikiwa ni mwezi mmoja tangu watwae Kombe la Dunia nchini Urusi
Aidha, Ujerumani ambayo ilifanya vibaya katika michuano ya Kombe la Dunia yenyewe imeshika nafasi ya 15 huku Argentina ikiwa nafasi ya 11 na Uhispania ikiangukia nafasi ya 09
Katika orodha hiyo Tanzania inashika nafasi ya 140 huku nchi ya Kwanza kwa Afrika ikiwa ni Tunisia ambayo inashika nafasi ya 24 kidunia
Kwa bara la Afrika, Tunisia imelingana alama na Senegal zote zikiwa nafasi ya 24 zikifuatiwa na Congo(37), Ghana(45) na Morocco(46).
0 COMMENTS:
Post a Comment