August 16, 2018


Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amesema Mwandishi Silas Mbise aliyepigwa na Polisi mnamo Agosti 08 katika Uwanja wa Taifa, alimkaba na kumtishia Askari baada ya kuzuiwa kuingia sehemu aliyokuwa haruhusiwi

Mbise ambaye ni Mwandishi wa Wapo Radio alipigwa na Polisi siku hiyo ya tamasha lililoandaliwa na Klabu ya soka ya Simba maarufu “Simba Day” ambalo klabu hiyo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana.

Aidha, IGP Sirro amesisitiza kuwa Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hilo na ulikamilika mwandishi huyo atafunguliwa mashitaka na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria

Hata hivyo, ameongeza kuwa Askari waliohusika kumpiga mwandishi huyo wanachunguzwa iwapo walitumia nguvu isiyohitajika na ikithibitika nao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi.

6 COMMENTS:

  1. That is the end of Story!!!
    Kesi ya Panya ikipelekwa kwa Paka matokeo yanajulikana. Hatuhitaji kuwashutumu askari wala kuwahoji waandishi habari walioshuhudia tukio hilo. Ikiwa wapo waliopiga video za Mbise akipigwa basi haikosekani video ya kuonesha Mbise akimkaba askari. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  2. Kumpiga mtu sio kitendo cha kiungwana. Hata kupigana pia sio kitendo cha mazingira yanayoleta taswira ya amani labda iwe upo katika mashindano halali ya ngumi. Wanahabari kwakuwa mmoja wao aliingia katika majaribu na polisi basi moja kwa moja waliwaaminisha watanzania na Dunia kuwa mwanahabari yule kapigwa bila kosa? Ni kama vile polisi wetu ni waendawazimu. Kisa kilihadithiwa on one side story na hakukuwa na copy ya maelezo ya upande wa pili yaani polisi kujieleza ilikuwaje? Nasema tena sikufurahia kitendo kile cha kupigwa mwanahabari na laani kwa namna yeyote ile ila mwanahabari anapojiona yupo juu kuliko vyombo vya ulinzi hapo lazima msuguano utatokea na kama kweli mwanahabari huyo aliamua kuingiana mwilini na askari kwakweli ni hatari kwani hata kwa hizo nchi tunazoziita za kidemokrasia na huru kufanya utakavyo uamuzi wa kwenda kumgusa polisi akiwa kazini hata kama kakukera basi ni sawa na jaribio la kutaka kujiua.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na pale chini akiwa mwandishi amelala akipigwa alikuwa kamkaba nani?

      Delete
  3. Mmmm Yaani askari alikabwa na mwandishi????.. Bila Shaka askari hakuvaa sare

    ReplyDelete
  4. Kwa hali ya kawaida hivi kweli Mbise amkabe askari, angekuwa na viungo vyake vyote? Dah!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic