August 31, 2018


Shirikisho la Soka nchini (TFF) limesema mpaka sasa halijajua zawadi ipi itatolewa kwa bingwa wa Ligi Kuu Bara mara baada ya msimu kumalizika.

Hatua hiyo imekuja kutokana na TFF kukosa mdhamini mkuu wa ligi baada ya aliyekuwa kujiengua.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Wilfred Kidao, amesema TFF bado inahangaika kusaka mdhamini mkuu kwa kufanya mazungumzo na makampuni mbalimbali ili kufanikisha hilo.

Kidao ameeleza uhakika wa kumpata mdhamini huyo utakuwepo kutokana na jithada ambazo wanazifanya kwa kipindi hiki.

TFF walishindwa kufikia mwafaka na kampuni ya mawasiliano, Vodacom iliyokuwa inadhimi ligi kwa muda mrefu ili kuongeza mkataba mwingine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic