August 17, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limefurahishwa na kiwango ambacho kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys kimeonesha katika mashindano ya CECAFA yanayoendelea hivi sasa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho hilo, Clifford Mario Ndimbo, amesema kwa kikosi kilichopo hivi sasa kinatoa imani kubwa ya kuendelea kufanya vizuri zaidi.

Hatua hiyo imekuja kufuatia Serengeti Boys kutoa dozi kali jana ya mabao 5-0 dhidi ya Sudan katika mchezo wa Kundi A ambalo ukiachilia Tanzania na Sudan lina timu zingine ambazo ni Burundi na Rwanda.

Clifford ameeleza vijana waliopo wamekuwa wakipambana na wao kama taasisi mama ya soka la Tanzania watazidi kukipa nguvu kuhakikisha kinazidi kufanya vema.

Katika kundi hilo, Serengeti Boys inaongoza ikiwa imecheza mechi mbili na kushinda zote huku ikiwa imejikusanyia alama 6 ikiwaacha Rwanda walio wa pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Burundi na Sudan mpaka sasa hazijapata alama zozote kutokana na kupoteza mechi zao mbili ambazo wameshacheza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic