August 3, 2018


Baada ya hivi karibuni baadhi ya watu kudai kuwa mchezaji mpya wa Coastal Union ya Tanga, Ally Salehe Kiba ‘Ali Kiba’ kuwa kanuni za Ligi Kuu Bara hazimruhusu kuitumikia timu hiyo katika ligi hiyo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa msimamo wake.

Ilidaiwa kuwa kanuni za ligi kuu hazimruhusu Kiba kuitumikia Coastal katika ligi hiyo kwa sababu ni mwanamuziki jambo ambalo lilizua maswali mengi kwa baadhi ya wapenzi na mashabiki wa soka hapa nchini.

Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madai ameliambia Championi Ijumaa kuwa, hakuna kanuni yoyote inayomzuia Ali Kiba asiitumikie Coastal Union katika michuano ya kwa sababu tu ni mwanamuziki.

Alisema mchezo wa soka haubagui, kila mtu anaruhusiwa kucheza. “Kanuni zetu hazijasema mchezaji lazima awe na kazi moja tu, anaweza kuwa mcheza mieleka, mcheza kikapu na mchezaji wa soka la ufukweni na kusajiliwa kucheza soka.

“Kwa hiyo, Coastal Union wao kama wameona kuwa Ali Kiba anaweza kuwasaidia hiyo ni juu yao ila hakuna kanuni inayomzuia kutoitumikia timu hiyo kwa sababu ya kazi yake,” alisema Madadi.

1 COMMENTS:

  1. Welcome come Ali Kiba to the football Industry unaweza wasokujua watalopka coz wanakalili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic