August 31, 2018




Na Mwandishi Wetu, Victoria, Nigeria
Tamasha la African Magic Viewers Choice Awards (AMVCA) linafanyika hapa katika miji ulio katika kisiwa cha Victoria na hii ni sehemu ya jiji la Lagos. Tuzo ambazo, watazamaji wanakuwa na nafasi kubwa kwa kuwa wanapiga kura kuwachagua ambao wanaamini ni washindi.
Multichoice, imekuwa ikifanya kazi kubwa kuhakikisha tuzo hizo chini ya chaneli maarufu zaidi ya filamu barani Afrika ya African Magic, imekuwa ikihakikisha kila kitu kinakwenda salama salimini.

Watanzania wawili wataiwakilisha Tanzania katika tuzo hizo ikiwa na kumbukumbu kushinda tuzo mbili katika tuzo za mara ya tano baada ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Single Mtambalike ‘Richie’ kila mmoja wao kuibuka na ushindi.

Hizi ni tuzo za mara ya sita na Watanzania watawakilishwa na Amil Issa Shivji, huyu ni kati ya watengeneza filamu bora kabisa ambaye hata tuzo za mwaka jana alikuwa hapa Victoria lakini bahati mbaya hakufanikiwa.
Shivji ni editor na ‘prodyuza’ mahiri, filamu za ‘Samaki Mchangani’ ni kati ya zilizompa sifa kubwa. Iliingia katika tuzo hizi mwaka jana haikushinda. Lakini bado ameendelea kufanya vema na filamu kama Who Killed Me na Shoesine, hii ilitoka mwaka 2013.

Matarajio makubwa ya yeye kufanya vizuri katika kipengeleza cha mtengeneza filamu bora huku Watanzania wakiwa na matumaini pia kwa Lester Millado.
Lester Millado, Mtanzania anayefanya kazi zake sehemu mbalimbali. Nyumbani Tanzania, Kenya na pia Canada. Mmoja wa wataalamu wa utengenezaji filamu katika mdumo wa Cinematography. 

MIllado amefanya vizuri na tamthilia ya T-Juncition ambaye imempa nafasi ya kuwania tuzo katika kipengele cha Best Cinematography/TV Series akichuana na Dickson Godwin na tamthilia ya Idemuze,  Rwamasigazi Kyakunzire (The Torture), Yinka Edward (Okafor Laws) na Akpe Ododoru (Tatu).
Inaweza ikawa nafasi nyingine kwa Watanzania hao kuiwakilisha Tanzania kwa mara nyingine ingawa wanaonekana kuwa katika ushindani mkubwa sana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic