August 21, 2018



Taarifa zimekuwa zikienea kwa kasi ya kimondo kwamba Manchester United inamtaka Zinedine Zidane kuchukua nafasi ya Kocha Jose Mourinho.

Lakini klabu ya Manchester United, imefunguka  na kusema haina nafasi za kazi na kusisitiza, haijawahi kuwasiliana na Zidane ,46, kocha wa zamani wa Real Madrid.

Baada ya kipigo cha mabao 3-2 ambacho walikipata Manchester United kutoka kwa Brighton, moto ukazidi kuwa mkali kuhusiana na nafasi ya Mourinho.

Chifu wa Man United, Ed Woodward ndiye aliyesema hawakufanya mazungumzo yoyote na Zidane kwa kuwa hawana nafasi ya kazi ya kocha mkuu kwa sasa.

Mourinho ,55, anaonekana yuko katika wakati mgumu katika kipindi hiki hasa kutokana na suala la Zidane kuendelea kuzungumzwa.

Huenda baada ya uongozi wa Manchester kuweka hadharani kwamba hauna mpango na Zidane, utapunguza presha kwa Mourinho lakini bado atatakiwa kukipa ushindi kikosi chake ili kufuta yanayoendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic