WACHEZAJI LIPULI MPAKA SASA HAWAJAKUTANA KAMBINI, MATOLA HUYU HAPA ANAELEZA SABABU
Na George Mganga
Wakati klabu nyingi nchini zikiwa zimeanza kujifua kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, uongozi wa Lipuli kutoka Iringa umesema wao bado hawajaanza mazoezi.
Kwa mujibu wa Seleman Matola ambaye ameachiwa kuingoza timu hiyo baada ya Kocha Mkuu, Amri Said kukimbilia Mbao FC, amesema sababu kubwa iliyosababisha kuchelewa kuanza mazoezi ni ukata.
Kwa mujibu wa Radio One, Matola ameeleza Lipuli imekuwa ikisumbuliwa na uhaba wa fedha ambao umesababisha hata wachezaji wenyewe washindwe kuwasili mapema kambini.
Kocha huyo amesema kuwa ukiachana na msimu huu, hata wakati wakijiandaa na msimu wa 2017/18 timu hiyo ilikuwa ikisumbuliwa na ukata huo lakini mwisho wa siku walipambana mpaka wakafikia hapo walipo.
"Mpaka sasa wachezaji wengi hawajawasili kambini, ni wachache wameanza kuja kutokana na ukata wa fedha, hata kuelekea msimu uliopita tulikuwa tukisumbuliwa na kukosekana kwa fedha, timu yetu haina wadhamini" alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment