August 1, 2018


Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Ibrahim Mkwawa, amewajibu baadhi ya wanachama Simba wanaopingana na katiba ya mwaka 2018 baada ya kufanyiwa usajili siku kadhaa zilizopita.

Mkwawa amesema wanachama hao kama wana malalamiko yenye maana wanapaswa kufuata taratibu rasmi za kupinga na si kuzungumza kwenye vyombo vya habari.

Msajili amesema katiba ya Simba ilijadiliwa katika mkutano mkuu wa klabu na kufuata taratibu ambapo pia ilipitia kunako makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na baadaye kuwalisishwa serikalini.

Mkwawa ameeleza kutokana na kufuata kila taratibu juu ya usajili wa katiba hiyo, ni rasmi sasa itatumika katika uchaguzi mkuu ujao Simba bila mapingamizi yoyote yale kutokana na kujikamilisha kwake.

Wanachama hao baadhi wamekuwa wakipingana na katiba hiyo kutokana na baadhi ya vipengele ikiwemo mgombea Urasi kutakuwa kuwa na kiwango cha elimu ya shahada badala ya kuishia kidato cha nne kama ilivyokuwa inayesma ya mwka 2014.

6 COMMENTS:

  1. Mimi nashangaa sana kuona hata baadhi ya viongozi wakuu wa zamani wa Simba kama Alhaj Rage anakipinga kipengele cha elimu ya Shahada. Hivi kweli dunia ya leo unataka klabu hizi kubwa nchini ziongozwe kama ilivyokuwa kwa wazee wetu wa miaka ya 1970? Tuwe wakweli tu. Uongozi wa sasa sio wa kujua kuongea tuu, elimu ya Chuo Kikuu ndio tunategemea atakuwa amesomea Uongozi,Utawala, Menejimenti,Uchumi, Masoko, Mahusiano (PR), nk. Hebu tuache kujidharau wenyewekama vile hatujui faida ya mtu aliyesoma vizuri. Hayo ndiyo mabadiliko tuyafanye.

    ReplyDelete
  2. Wapuuzi hawo ...njaa zinawasumbua

    ReplyDelete
  3. yani wameanza tena mambo yao ya ajabu timu ndo inasukwa wanaanza kuleta mambo yasiyo kua Na maana kama shida yao ni Kiki wakachukue kwenye pikipiki

    ReplyDelete
  4. hiyo timu ilianzishwa na watu wasio na elimu hao wanaojiita wasomi wakaanzishe timu yao na sio kuleta usomi kwenye timu ambayo ilianzishwa na mangumbaru wasio na elimu

    ReplyDelete
  5. Kwa hiyo kama ilianzishwa na wasiosoma ndiyo tuendelee nao?wewe ni kandambili tumekubaini. Basis hata makanisani tusiende kwani mwanzo tuliabudu msituni,jinga wewe

    ReplyDelete
  6. Tumeingia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji timu uaohitaji timu kuendeshwa kisasa na hivyo watu wenye elimu wanahitajika cha ajabu bado watu wanataka kuongozwa na wauza chipsi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic