August 1, 2018


Baadhi ya wanachama wa Simba wameipokea katiba mpya ambayo imetoka kusajiliwa hivi karibuni na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Ibrahim Mkwawa katika makao makuu ya klabu hiyo.

Licha ya kuipokea katiba hiyo, wanachama hao wamepingana na baadhi ya vipengele ambavyo wameeleza kuwa havikuwa katika makubalino ya pande mbili baina ya viongozi na upande wao.

Kwa mujibu wa Radio One, Mwanamachama mmoja anayejulikana kwa jina la Mussa Said kutoka tawi la Simba Tishio, amesema kuwa kipengele cha kumtaka mgombea Urais kuwa na kiwango cha elimu ya shahada haikujadiliwa pamoja.

Aidha ameeleza pia kipengele kingine ni kuhusiana na kuhusiana na wajumbe ambao wanapaswa kuwa na elimu ya kiwango cha elimu ya kidato cha nne, akisema kuwa si jambo sahihi.

Wakati Said akilalamikia na kuhoji juu ya katiba hiyo iliyosajiliwa mwaka huu 2018, malalamishi yake yanakuwa kama ynakosa nguvu kutokana na Msajili Mkuu kutoka Serikalini, Mkwawa, kuipitisha katiba hiyo kuwa ndiyo itatumika kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Klabu ya Simba kupitia viongozi wake watakutana Agosti 31 kwa ajili ya kuandaa Kamati maalum ya Uchaguzi kuanza mchakato rasmi wa kuwapata viongozi watakaoweza kuiongoza klabu kwa miaka minne ijayo.

10 COMMENTS:

  1. Mimi nashangaa sana kuona hata baadhi ya viongozi wakuu wa zamani wa Simba kama Alhaj Rage anakipinga kipengele cha elimu ya Shahada. Hivi kweli dunia ya leo unataka klabu hizi kubwa nchini ziongozwe kama ilivyokuwa kwa wazee wetu wa miaka ya 1970? Tuwe wakweli tu. Uongozi wa sasa sio wa kujua kuongea tuu, elimu ya Chuo Kikuu ndio tunategemea atakuwa amesomea Uongozi,Utawala, Menejimenti,Uchumi, Masoko, Mahusiano (PR), nk. Hebu tuache kujidharau wenyewekama vile hatujui faida ya mtu aliyesoma vizuri. Hayo ndiyo mabadiliko tuyafanye.

    ReplyDelete
  2. Wataizoea tu, wanaadamu tuna tabia ya kuishi na mazoea kila jipya kwetu linakuwa gumu kulipokea lakini watazoea tu na watasahau ya kale.....mabadiliko yanahitajika kwa maendeleo ya Simba yetu na mpira wetu...narudia tena mtazoea tu wapibgaji

    ReplyDelete
  3. Atutaki kinakayumba katiba tuliibadili pamoja iwejeleo muipinge wakati timu imeshakua kampuni

    ReplyDelete
  4. Simba ni taasisi kubwa Now na tunamalengo makubwa sana hujasoma kaa pembeni... Mbona ata vigezo vya elimu ni vidogo sanaa

    ReplyDelete
  5. Simba ni taasisi kubwa Now na tunamalengo makubwa sana hujasoma kaa pembeni... Mbona ata vigezo vya elimu ni vidogo sanaa

    ReplyDelete
  6. Hata ukiwaangalia hao wanaopinga muonekano wao tu majibu unayapata siyo watu wa maendeleo ni wapigaji tu hata kiwango cha elimu kinacholalamikiwa bado ni kidogo

    ReplyDelete
  7. PENGINE inawezekana malalamiko yao ni ya msingi sana. Lakini walikuwa wapi muda wote huo?
    Anyways; Hii hoja ya kupinga kigezo fulani cha elimu ni uthibitisho kuwa bado tunasafari ndefu sana..!!

    ReplyDelete
  8. Simba ni taasisi kubwa na kwa mfumo wa sasa tunahitaji kiongozi mwenye elimu na uwezo wa kulisongesha jahazi mbele kwa mbele

    ReplyDelete
  9. nimemuona huyo Said aliyekuwa akilalamika jana, bado kijana mdogo sana...anaweza kujiendeleza pia na kufikia kiwango hicho cha elimu kama bado ana ndoto za kuja kuwa kiongozi wa simba, vinginevyo ni vyema akawa shabiki tu...

    ReplyDelete
  10. Simba in a malengo makubwa inahitaji watu makini wenye elimu upeo mpana na mikakati ya kuifikisha simba kimataifa hao wanaopinga ni mashabiki tu ambao wanamahaba na timu ila hawana malengo ya kuitoa simba ilipo wao mi naona kila mmoja abaki kwenye nafasi yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic